http://www.vessella.it KARIBU!
Jifunze lugha ya Kiesperanto

YALIYOMO

•  Utangulizi
•  Somo la kwanza
•  Somo la pili
•  Somo la tatu
•  Somo la nne
•  Somo la tano
•  Somo la sita
•  Somo la saba
•  Somo la nane
•  Somo la tisa
•  Somo la kumi

•  Kamusi

UTANGULIZI

Madhumuni ya kitabu hiki ni kuwawezesha wale Waafrika wanaojua kusoma Kiswahili kujifunza lugha ya Kiesperanto bila mwalimu. (Kiesperanto ni nini?)

Litakuwa jambo la busara sana kwa wanafunzi kusoma kidogo kidogo kila siku, bila kusoma haraka kitabu kizima, na pia wao wafanye mazoezi yote katika kitabu hiki kwa kufuata mpango wa kitabu chenyewe. Katika kila zoezi kuna mfano unaowaonyesha wanafunzi namna ya kufanya zoezi lenyewe. Zaidi ya hayo wanafunzi watanufaika wakipeleka kazi zao kwa "UNIVERSALA ESPERANTO-­ASOCIO", ili mwalimu awaongoze kwa kuyasahihisha majibu yao. Anayejifunza akiyafuata masomo haya atafikia kiwango cha msingi cha ujuzi wa Kiesperanto. Kiwango cha upeo kitafikia kwa kufuata masomo ya kitabu kingine.

Maneno ya kisarufi yaliyomo katika kitabu hiki yanabainishwa katika KAMUSI YA KISWAHILI SANIFU, iliyotungwa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na iliyochapishwa na Oxford University Press ya Dar es Salaam na Nairobi mnamo 1981, kwa hiyo litakuwa jambo la busara kujipatia kamusi hiyo, lakini katika kitabu hiki kila neno la kisarufi linabainishwa tena. Anayekuta shida yoyote tafadhali tuandikie barua.

Ĉi tiu Iernolibro estas adapto de "Esperanto for beginners” verkita de M. C. Butler.

Mi tamen ne menciis la nomon de Butler sur la koverto por demeti de li ĉian respondecon pri la enhavo de ĉi tiu sŭahila versio. Fakte la de mi faritaj ŝanĝoj - ĉefe en la gramatikaj klarigoj - devontigas nur min porti la respondecon de ĉi tiu "Jifunze lugha ya Kiesperanto".

Batla estas ĉiakaze la metodo.

Nino Vessella
Latina (Italujo)
Somero 1982

 


© Nino Vessella, 1996-.
Diritti riservati. Nessuna parte può essere riprodotta, in qualsiasi forma o mezzo, senza citare la fonte.
Ĉiuj rajtoj rezervitaj. Neniu parto povas esti reproduktita, en kiu ajn formo au per kiu ajn metodo, sen mencii ĉi tiun fonton.
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kunakili sehemu yoyote bila kuitaja asili yake hii.
All rights reserved. No part may be reproduced, in any form or by any means, without mention of this source.