Ujerumani
|
|||||
Kaulimbiu ya taifa: Einigkeit und Recht und Freiheit (Kijerumani: "Umoja na Haki na Uhuru”) |
|||||
Wimbo wa taifa: Wimbo wa Wajerumani (beti ya tatu) Umoja na Haki na Uhuru |
|||||
Mji mkuu | Berlin |
||||
Mji mkubwa nchini | Berlin | ||||
Lugha rasmi | Kijerumani 1 | ||||
Serikali | Shirikisho la Jamhuri Joachim Gauck Angela Merkel |
||||
Dola Takatifu la Kiroma Dola la Ujerumani Shirikisho la Jamhuri Maungano |
843 (Mkataba wa Verdun) 18 Januari 1871 23 Mei 1949 3 Oktoba 1990 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
357,050 km² (ya 63) 2.416 |
||||
Idadi ya watu - 2014 kadirio - 2011 sensa - Msongamano wa watu |
80,716,000 (ya 16) 80,219,695 226/km² (ya 58) |
||||
Fedha | Euro (€) 2 (EUR ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) |
||||
Intaneti TLD | .de | ||||
Kodi ya simu | +49 |
||||
1 Kideni, Kijerumani cha Kaskazini, Kisorbia, Kifrisia ni lugha rasmi katika mikoa kadhaa 2 hadi 1999: Mark (DM) |
Ujerumani (pia: Udachi, kwa Kijerumani: Deutschland) ni nchi ya Ulaya ya Kati.
Imepakana na Denmark, Poland, Ucheki, Austria, Uswisi, Ufaransa, Luxemburg, Ubelgiji na Uholanzi.
Ni nchi yenye watu wengi katika Ulaya, isipokuwa Urusi ina watu zaidi.
Uchumi wa Ujerumani una uwezo mkubwa: ni nchi inayouza bidhaa nyingi nje kushinda mataifa yote ya dunia.
Muundo wake kiutawala ni shirikisho la jamhuri lenye majimbo 16 ndani yake na kila jimbo lina kiwango cha kujitawala.
Lugha asilia ni Kijerumani kinachojadiliwa kwa lahaja mbalimbali, lakini wenyeji wote wanasikilizana. Katika maeneo mawili kuna wasemaji asilia wa Kideni na Kisorbia.
Wahamiaji wa karne ya 20 wameleta lugha zao, hasa Kituruki na lugha za Ulaya ya Kusini.
Upande wa dini, Wakristo ni 66.8% (Wakatoliki 30.8%, Walutheri 30.3%, Waprotestanti wengine 5.7%), huku Waislamu wakiwa 1.9%. Thuluthi moja ya wakazi haina dini yoyote.
Jina la nchi
Wenyeji wanaiita "Deutschland" ( Deutschland (info), tamka: doich-land) na jina hilo limeingia katika Kiswahili kama "Udachi". Lilikuwa jina la kawaida katika karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20.
Siku hizi neno "Ujerumani" limechukua nafasi yake kutokana na Kiingereza kinachoiita "Germany".
Jiografia
Ujerumani unaenea kati ya bahari upande wa kaskazini na milima ya Alpi upande wa kusini.
Mipaka yake upande wa magharibi na mashariki ilibadilika mara nyingi katika historia yake; tangu mwaka 1945 mpaka wa mashariki ni mto Oder. Upande wa magharibi sehemu ya mpaka ni mto Rhein.
Kuna kanda tatu za kijiografia:
Tambarare ya pwani ya kaskazini ni eneo bapa; hakuna milima na nchi haipandi juu ya mita 200, sehemu kubwa ni kati ya uwiano wa bahari na mita 60 juu yake.
Historia
- Dola Takatifu la Kiroma (900-1806)
- Shirikisho la Ujerumani (1815-1866)
- Dola la Ujerumani (1871-1945)
- Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani (1949 hadi 1990 Ujerumani wa Magharibi)
- Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani (1949 hadi 1990 Ujerumani wa Mashariki)
Miji
Majiji yenye wakazi zaidi ya milioni moja ni:
Miji mikubwa mingine ni:
Majimbo
- Baden-Württemberg
- Bavaria (Freistaat Bayern)
- Berlin
- Brandenburg
- Bremen (Freie Hansestadt Bremen)
- Hamburg (Freie und Hansestadt Hamburg)
- Hesse (Hessen)
- Mecklenburg-Pomerini (Mecklenburg-Vorpommern)
- Saksonia Chini (Niedersachsen)
- Rhine Kaskazini-Westfalia (Nordrhein-Westfalen)
- Rhine-Palatino (Rheinland-Pfalz)
- Jimbo la Saar (Saarland)
- Saksonia (Freistaat Sachsen)
- Saksonia-Anhalt (Sachsen-Anhalt)
- Schleswig-Holstein
- Thuringia (Freistaat Thüringen)
Watu maarufu
- Alberto Mkuu
- Johann Sebastian Bach
- Michael Ballack
- Ludwig van Beethoven
- Papa Benedikto XVI
- Johannes Brahms
- Johann Wolfgang von Goethe
- Günter Grass
- Johannes Gutenberg
- Georg Wilhelm Friedrich Hegel
- Hildegarda wa Bingen
- Adolf Hitler
- Immanuel Kant
- Martin Luther
- Karl Marx
- Wolfgang Amadeus Mozart
- Friedrich Nietzsche
- Valentin Weigel
Nchi za Umoja wa Ulaya | |
---|---|
Austria | Bulgaria | Denmark | Estonia | Hispania | Hungaria | Ireland | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituania | Luxemburg | Malta | Poland | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Ufalme wa Muungano | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi |
|
Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ujerumani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |