Siasa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Siasa ni njia ya kufanya maamuzi katika taifa, mji au hata dunia nzima (siasa ya kimatatifa).

Sehemu muhimu ya siasa ni majadiliano kati ya watu mbalimbali wenye nguvu au mamlaka.

Katika demokrasia kila mtu ana kiasi fulani cha nguvu, kwa hiyo siasa ya demokrasia ina maana ya watu wote kuchangia maamuzi.

Hapa chini, mifumo mingine ya kisiasa huelezwa kifupi:

Utawala wa Kifalme[hariri | hariri chanzo]

ni mfumo wa uongozi unaompa mamlaka ya dola na ya serikali Mfalme. Katika mfumo huu madaraka hurithiwa na mtu wa familia ya kifalme.

Utawala wa Kiimla[hariri | hariri chanzo]

ni mfumo wa uongozi unaotoa madaraka yasiyo na mipaka kwa kiongozi. Katika utawala huu watu binafsi hawana haki na uhuru katika maamuzi.

Utawala finyu[hariri | hariri chanzo]

ni mfumo unaowapa wachache nguvu za maamuzi katika dola na serikali. Nafasi ya wachache hawa hutokana na haiba na uwezo wao kiuchumi, kijamii, kijeshi au kutokana na mafanikio yao katika nyanja mbalimbali za maisha. Mfumo huu ni nadra sana siku za hivi karibuni. Pia waweza kuitwa utawala wa makabaila.

Utawala wa Umma[hariri | hariri chanzo]

ni utawala unaotokana na jamii kuamua misingi ya kujiongoza. Mfumo huu wa utawala hujulikana kama Utawala wa Kidemokrasia na umegawanyika katika sehemu nne.

Demokrasia Baguzi[hariri | hariri chanzo]

ni aina ya Demokrasia inayojikita katika kulinda nguvu za kiuchumi zaidi.

Demokrasia Duni[hariri | hariri chanzo]

ni aina ya demokrasia inayotokana na makundi ya watu na kisha kupitia makundi hayo watu kuunda serikali mfano: chama - serikali.

Demokrasia Endelevu[hariri | hariri chanzo]

ni aina ya demokrasia inayotoa fursa ya usawa na kupinga matabaka katika jamii.

Demokrasia Shirikishi[hariri | hariri chanzo]

katika aina hii ya Demokrasia wachache hupewa dhamana na wengi katika uwakilishi wa jamii katika maamuzi.

Wachache uchaguliwa na wengi kwa njia ya Demokrasia huru na haki kwa kufuata Katiba ya nchi hiyo. Mfano: Wabunge uwakilisha wananchi wao katika kuleta maendeleo na kuishauri serikali juu ya maendeleo ya nchi.

Demokrasia[hariri | hariri chanzo]

ni mfumo unatoa fursa ya madaraka kwa umma moja kwa moja au kutokana na kuwakilishwa.