Uswidi
|
|||||
Kaulimbiu ya taifa: För Sverige i tiden1 (Kiswahili: "Kwa Uswidi, wakati wake") |
|||||
Wimbo wa taifa: Du gamla, du fria ("Wewe kizee,wewe huru") |
|||||
Mji mkuu | Stockholm |
||||
Mji mkubwa nchini | Stockholm | ||||
Lugha rasmi | None Kiswidi de facto2 |
||||
Serikali | Ufalme wa kikatiba Carl XVI Gustaf Stefan Löfven |
||||
Kuungana kwa nchi {{{established_events}}} |
{{{established_dates}}} | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
449,964 km² (55) 8.67% |
||||
Idadi ya watu - 2014 kadirio - 2013 sensa - Msongamano wa watu |
9,716,962 (31 Agosti 2014) [1] (89) |
||||
Fedha | Swedish krona (SEK ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) |
||||
Intaneti TLD | .se | ||||
Kodi ya simu | +46 |
||||
1 För Sverige i tiden ni wito la mfalme Carl XVI Gustaf 2 Kiswidi ni lugha ya ktaifa hali halisi. Lugha tano zimekubaliwa rasmi kama lugha za vikundi vidogo ndani ya taifa. |
Uswidi (au: Sweden; Swideni; kwa Kiswidi: "Sverige") ni nchi ya Skandinavia katika Ulaya ya Kaskazini. Imepakana na Ufini (Finland) na Norwei.
Ina pwani ndefu kwenye bahari ya Baltiki. Kuna daraja la kuvukia mlango wa bahari ya Oresund ya kuunganisha Uswidi na Denmark.
Uswidi ni nchi kubwa yenye wakazi wachache ni milioni 9.7 pekee, wengi wao wenye asili ya makabila ya Kijerumani. Kuna misitu mikubwa sana na maziwa mengi.
Upande wa dini, 67.5% ni Walutheri, lakini 2% tu wanashiriki ibada ya kila wiki.
Siasa[hariri | hariri chanzo]
Uswidi ni ufalme wa kikatiba yaani Mkuu wa Dola ni mfalme (kwa sasa Carl XVI Gustaf), lakini huyu mfalme anapaswa kufuata sheria ya katiba ya nchi. Utawala umo mikononi mwa serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.
Katika karne ya 20 Uswidi umefaulu vizuri kujenga uchumi ili kuondoka katika umaskini na kuwa moja kati ya nchi tajiri za dunia.
Nchi ilijiunga na Umoja wa Ulaya mwaka 1995 lakini haikukubali pesa ya Euro ikaendelea na Krona ya Uswidi.
Jiografia[hariri | hariri chanzo]
Nchi imegawiwa katika mikoa mitatu: Norrland katika Kaskazini, Svealand katikati na Götaland katika kusini.
Hali ya hewa ya sehemu kubwa ya Uswidi si baridi kutokana na athira ya mkondo wa Ghuba. Kuna tofauti kati ya urefu wa mchana katika miezi ya Mei hadi Julai na giza wakati wa Desemba. Tarehe 21 Juni ni siku ndefu: hakuna giza kabisa na usiku wake Waswidi hufanya sherehe kubwa ya "midsommar" kwa ngoma na dansi kote nchini.
Picha za Uswidi[hariri | hariri chanzo]
-
Kebnekaise ni mlima mkubwa wa Uswidi
-
Delta ya Rapa katika hifadhi ya taifa ya Sarek ni sehemu ya Urithi wa Dunia wa Laponia.
-
Wanyamapori wakubwa wa Uswidi ni mbawala wakubwa
-
Stockholm – mji wa kale
-
Midsommar (mchoro wa Anders Zorn, 1897)
-
Mti wa sherehe ya „midsommar“
Wilaya[hariri | hariri chanzo]
Län | Herufi | Mji mkuu | Eneo | Ramani |
---|---|---|---|---|
Blekinge län | K | Karlskrona | 2.947 km² | |
Dalarnas län | W | Falun | 28.196 km² | |
Gotlands län | I | Visby | 3.151 km² | |
Gävleborgs län | X | Gävle | 18.200 km² | |
Hallands län | N | Halmstad | 5.462 km² | |
Jämtlands län | Z | Östersund | 49.343 km² | |
Jönköpings län | F | Jönköping | 10.495 km² | |
Kalmar län | H | Kalmar | 11.219 km² | |
Kronobergs län | G | Växjö | 8.467 km² | |
Norrbottens län | BD | Luleå | 98.249 km² | |
Skåne län | M | Malmö | 11.035 km² | |
Stockholms län | AB | Stockholm | 6.519 km² | |
Södermanlands län | D | Nyköping | 6.103 km² | |
Uppsala län | C | Uppsala | 8.208 km² | |
Värmlands län | S | Karlstad | 17.591 km² | |
Västerbottens län | AC | Umeå | 55.190 km² | |
Västernorrlands län | Y | Härnösand | 21.685 km² | |
Västmanlands län | U | Västerås | 5.145 km² | |
Västra Götalands län | O | Göteborg | 23.956 km² | |
Örebro län | T | Örebro | 8.546 km² | |
Östergötlands län | E | Linköping | 10.645 km² | |
Jumla | 410.977 km² |
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
Nchi za Umoja wa Ulaya | |
---|---|
Austria | Bulgaria | Denmark | Estonia | Hispania | Hungaria | Ireland | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituania | Luxemburg | Malta | Poland | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Ufalme wa Muungano | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi |
|
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Uswidi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |