Gambia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Republic of The Gambia
Bendera ya Gambia Nembo ya Gambia
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Progress, Peace, Prosperity (Maendeleo, Amani, Ustawi)
Wimbo wa taifa: For The Gambia Our Homeland (Kwa Gambia nchi yetu)
Lokeshen ya Gambia
Mji mkuu Banjul
13°28′ N 16°36′ W
Mji mkubwa nchini Serrekunda
Lugha rasmi Kiingereza
Serikali Jamhuri
Yahya Jammeh
Uhuru
Kutoka Uingereza
18 Februari 1965
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
10,689 km² (ya 164)
11.5
Idadi ya watu
 - Julai 2005 kadirio
 - 2013 sensa
 - Msongamano wa watu
 
1,593,256 (ya 150)
1,882,450
171.1/km² (ya 74)
Fedha Dalasi (GMD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
GMT (UTC)
(UTC)
Intaneti TLD .gm
Kodi ya simu +220

-


Map of the Gambia

Gambia (jina rasmi: Republic of The Gambia) ni nchi ndogo kabisa ya Afrika bara. Eneo lake linazungukwa na Senegal kwa kufuata mwendo wa mto Gambia.

Kimsingi nchi yote ni maeneo mawili kandokando ya mto huo; urefu ni takriban km 500, upana kati ya 10 na 50.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Nchi imepatikana kutokana na mvutano kati ya Uingereza na Ufaransa wakati wa ukoloni.

Mwanzoni Uingereza ulitafuta tu njia ya maji kwa ajili ya biashara, bila kujali utawala wa nchi.

Mapatano kati ya Ufaransa na Uingereza baada ya vita vya Napoleon Bonaparte yaliimarisha hali hiyo. Wafaransa walichukua eneo lote kubwa la Senegal, na Waingereza ile kanda ndogo ndani ya Senegal.

Tangu uhuru wa nchi zote mbili palikuwa na mpango wa kuziunganisha kwa njia ya shirikisho lakini Gambia ilitoka katika mapatano hayo mwaka 1989.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wa nchi ni hasa wa kabila la Wamandinka, halafu Wafulani na Wawolof, jumla milioni 1.9 hivi.

Makabila ya Gambia
asilimia Kabila
42 % Wamandinka
18 % Wafula
16 % Wawolof-Waserer
10 % Wadiola
9 % Waserahuli
1 % Wamanjago
1 % Waaku
0,4 % Wabamana
0,9 % wengine
Namba za mwaka 2003

Lugha rasmi ni Kiingereza.

Upande wa dini, Uislamu unafuatwa na 90% za wakazi, Ukristo (hasa Kanisa Katoliki) na 8%, wakati wafuasi wa dini asilia za Kiafrika ni 2%.

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Bennet, Lindsey and Voormeij, Lisa, The Gambia (Travellers), (Thomas Cook Publishing, 2009)
  • Emms, Craig and Barnett, Linda, Gambia (Bradt Travel Guides), (Bradt Travel Guides, 2006)
  • Hughes, Arnold, Historical Dictionary of the Gambia, (Scarecrow Press, 2008)
  • Hughes, Arnold and Perfect, David, A Political History of The Gambia, 1816–1994, (University of Rochester Press, 2008)
  • Gregg, Emma and Trillo, Richard, The Rough Guide to The Gambia, (Rough Guides, 2006)
  • Kane, Katharina, Lonely Planet Guide: The Gambia and Senegal, (Lonely Planet Publications, 2009)
  • Rice, Berkeley, Enter Gambia: The Birth of an Improbable Nation, (Houghton Mifflin. 1967)
  • Sarr, Samsudeen, Coup D'etat by the Gambia National Army, (Xlibris, Corp., 2007)
  • Sternfeldt, Ann-Britt, The Good Tourist in The Gambia: Travelguide for conscious tourists Translated from Swedish by Rolli Fölsch (Sexdrega,2000)
  • Tomkinson, Michael, Michael Tomkinson's Gambia, (Michael Tomkinson Publishing, 2001)
  • Various, Insight Guide: Gambia and Senegal, (APA Publications Pte Ltd., 2009)
  • Wright, Donald R, The World and a Very Small Place in Africa: A History of Glogalization in Niumi, The Gambia (New York: M.E. Sharpe, 2004)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Serikali
Taarifa za jumla
Afya
Utalii
Biashara


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia
Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Gambia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.