Bahrain

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
مملكة البحرين
Mamlakat al-Bahrayn

Ufalme wa Bahrain
Bendera ya Bahrain Nembo ya Bahrain
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Bahrainona
Wimbo wa taifa: بحريننا  (Bahrainona)
"Bahrain yetu"
Lokeshen ya Bahrain
Mji mkuu Manama
26°13′ N 50°35′ E
Mji mkubwa nchini Manama
Lugha rasmi Kiarabu
Serikali Ufalme wa kikatiba
Hamad Bin Isa Al Khalifa
Khalifah ibn Sulman Al Khalifah
Salman Bin Hamad Al Khalifa
Uhuru
tarehe
15 Agosti 1971
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
665 km² (ya 189)
0
Idadi ya watu
 - 2005 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
698,585a (ya 164)
987/km² (ya 10)
Fedha Bahraini Dinar (BHD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+3)
(UTC)
Intaneti TLD .bh
Kodi ya simu +973

-

a Includes 235,108 non-nationals (Julai 2005 estimate).


Ramani ya visiwa vya Bahrain
Bahrain inavyoonekana kutoka angani

Bahrain (kwa Kiarabu: مملكة البحرين Mamlakat al-Baḥrayn, Ufalme wa Bahrain) ni nchi ya visiwa na ufalme mdogo katika Ghuba ya Uajemi karibu na pwani ya Saudi Arabia.

Nchi ni tajiri kutokana na mapato ya mafuta ya petroli.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Bahrain iko upande wa mashariki wa Bara Arabu.

Eneo lake lina visiwa 33. Vikubwa kati ya hivyo ni:

  • Kisiwa kikuu cha Bahrain chenye urefu wa km 48 na upana wa km 16: kina 85% za eneo lote la ufalme na ni mahali pa mji mkuu Manama. Kimeunganishwa kwa daraja na:
  • kisiwa cha Muharraq (chenye 18 km²) penye uwanja wa ndege.
  • funguvisiwa ya Hawar (50 km²) karibu na pwani ya Qatar.
  • kisiwa cha Umm Na'san (19 km²) kisicho na wakazi wa kudumu kwa sababu hakina maji; barabara inayounganisha Bahrain na Saudia kwa njia ya daraja inapita hapo.
  • kisiwa cha Sitra (10 km²) kimeunganishwa pia kwa daraja na kisiwa kikuu; pana viwanda hapo.

Nchi ni tambarare; kilima cha juu ni Jabal ad-Dukhan chenye m 137 juu ya UB.

Sehemu kubwa ya eneo ni jangwa, lakini kaskazini mwa kisiwa kikuu pana visima na kilimo cha bustani na mitende.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wengi ni wahamiaji kutoka nchi nyingi duniani, wakiwa na lugha na dini mbalimbali.

Wenyeji ni Waarabu Waislamu, ila upande wa madhehebu wamegawanyika kati ya Washia na Wasuna.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Uchumi wa Bahrain hutegemea hasa mafuta ya petroli yanayozalisha 30% ya pato la taifa na 60% za mapato yote ya serikali. Serikali imejitahidi kujenga matawi mengine ya uchumi hasa viwanda vinavyotumia mafuta kwa kutengeneza bidhaa za aina nyingi pamoja na biashara.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bahrain kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China.