Amerika ya Kusini
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Amerika ya Kusini ni bara upande wa Kusini mwa Ikweta. Inapakana na Bahari ya Pasifiki upande wa Magharibi, na Bahari ya Atlantiki upande wa Mashariki.
Katika bara hilo kuna nchi zifuatazo:
- Argentina
- Bolivia
- Brazil
- Chile
- Ekuador
- Guyana
- Guyana ya Kifaransa
- Kolombia
- Paraguay
- Peru
- Surinam
- Uruguay
- Venezuela
Urithi wa ukoloni: Lugha na utamaduni[hariri | hariri chanzo]
Kwa lugha mablimbali bara inahesabiwa katika "Amerika ya Kilatini" kwa sababu wakazi wengi hutumia lugha za Kirumi hasa Kihispania na Kireno zilizizotokana na Kilatini.
Sababu yake ni ya kwamba sehemu kubwa ya bara hii ilikuwa koloni ya Hispania. Brazil ilikuwa koloni ya Ureno. Nchi zote mbili ziliacha tabia za utamaduni wao pamoja na lugha zilizokuwa lugha za kitaifa.
Nchi za Guyana pekee zilikuwa koloni za mataifa mengine ya Ulaya zilizoacha lugha zao:
- Guyana ilikuwa koloni ya Uingereza ikitumia Kiingereza (zamani illitwa Guyana ya Kiingereza)
- Surinam ilikuwa koloni ya Uholanzi ikitumia Kiholanzi (zamani illitwa Guyana ya Kiholanzi)
- Guyana ya Kifaransa ilikuwa koloni ya Ufaransa imekuwa mkoa wa Ufaransa na sehemu ya Umoja wa Ulaya ikitumia Kifaransa.
Orodha ya nchi na maeneo[hariri | hariri chanzo]
Jina la nchi au eneo, bendera |
Eneo (km²) |
Wakazi (2007) |
Wakazi kwa km² | Mji mkuu |
---|---|---|---|---|
Argentina | 2,766,890 | 40,677,348 | 14.3 | Buenos Aires |
Bolivia | 1,098,580 | 9,247,816 | 8.1 | La Paz, Sucre |
Brazil | 8,514,877 | 191,908,598 | 22.0 | Brasilia |
Chile | 756,950 | 16,454,143 | 21.1 | Santiago de Chile |
Kolombia | 1,138,910 | 45,013,674 | 37.7 | Bogotá |
Ekuador | 283,560 | 13,927,650 | 47.1 | Quito |
Falkland Islands (Ufalme wa Muungano) | 12,173 | 3,140[1] | 0.26 | Port Stanley |
Guyana ya Kifaransa (Ufaransa) | 91,000 | 221,450 (Jan. 2008)[2] | 2.7 | Cayenne |
Guyana | 214,970 | 770,794 | 3.6 | Georgetown |
Paraguay | 406,750 | 6,347,884 | 15.6 | Asunción |
Peru | 1,285,220 | 28,220,764 | 21.7 | Lima |
Visiwa vya South Georgia na South Sandwich (Ufalme wa Muungano) |
3,093 | 20 | 0 | Grytviken |
Surinam | 163,270 | 438,144 | 2.7 | Paramaribo |
Uruguay | 176,220 | 3,477,778 | 19.4 | Montevideo |
Venezuela | 912,050 | 26,414,815 | 27.8 | Caracas |
Jumla | 17,824,513 | 382,426,313 | 21.5 |
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Falkland Islands: July 2008 population estimate. CIA World Factbook.
- ↑ Population des régions au 1er janvier. INSEE. Iliwekwa mnamo 2009-01-20.
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Amerika ya Kusini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |