Sudan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
جمهورية السودان
Jumhuriyat as-Sudan

Republic of the Sudan
Bendera ya Sudan Nembo ya Sudan
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Al-Nasr Lana (Kiarabu: Ushindi ni Wetu)
Wimbo wa taifa: نحن جند للہ جند الوطن Nahnu Jund Allah Jund Al-watan ("Sisi ni Jeshi ya Mungu na Nchi yetu")
Lokeshen ya Sudan
Mji mkuu Khartoum
15°00′ N 30°00′ E
Mji mkubwa nchini Omdurman
Lugha rasmi Kiarabu
Serikali
Rais

Omar al-Bashir
Uhuru
 - Tarehe
Kutoka Misri na Uingereza
1 Januari 1956
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
1,886,068 km² (ya 16)
5%
Idadi ya watu
 - Julai 2014 kadirio
 - 2008 sensa
 - Msongamano wa watu
 
37,289,406 (ya 35)
30,894,000
16.4/km² (195)
Fedha Dinar (SDD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
MSK (UTC+3)
not observed (UTC+3)
Intaneti TLD .sd
Kodi ya simu +249

-


Ramani ya Sudan ikionyesha majimbo yake

Jamhuri ya Sudan, ama Sudan ni nchi kubwa ya tatu ya Afrika kulingana na eneo.

Imepakana na Misri kaskazini, Bahari ya Shamu kaskazini-mashariki, Eritrea na Ethiopia mashariki, Sudan Kusini kusini-mashariki, Afrika ya Kati na Chadi magharibi, na Libya kaskazini-magharibi.

Kijiografia nchi hii huhesabiwa kama sehemu ya Afrika ya Kaskazini.

Mji mkuu ni Khartoum.

Majimbo ya Sudan Kusini yalikuwa sehemu ya nchi hiyo lakini yalipiga kura ya kujitenga yakapata kuwa nchi huru kuanzia tarehe 9 Julai 2011.

Aliyekuwa makamu wa Rais John Garang, ambaye awali aliongoza wanamgambo wa Sudan ya Kusini kupigania uhuru wa majimbo ya kusini.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Mlima wa Dair eneo ya kati, Sudan
Bwawa kusini Sudan

Sudan iko upande wa Afrika ya kaskazini, ina pwani kwenye bahari ya Shamu kati ya Misri na Eritrea. Imetamalikiwa zaidi na mto Nile na mikono yake.

Kwa eneo ya kilomita mraba 1,886,068 (728,215 sq mi), ni nchi ya tatu kwa ukubwa katika bara la Afrika na ya kumi na sita duniani.

Ardhi yenyewe ni kiwara, lakini kuna milima upande wa mashariki na magharibi.

Hali ya anga ni ya mwangaza kusini, na mikuranga kaskazini.

Mvua yapatikana mwezi wa Aprili na Oktoba.

Uharibifu wa mazingira hasa ni kwa sababu ya mmomonyoko wa udongo na utapakazi wa jangwa.

Majimbo[hariri | hariri chanzo]

Ona pia: Orodha ya miji Sudan

Historia[hariri | hariri chanzo]

Sanamu ya Mfalme wa Wanubi, Sudan
Muhammad al-Mahdi
Dola la Mahdi 1881-1898

Historia ya awali[hariri | hariri chanzo]

Nchi ilikuwa na makazi ya kudumu kuanzia milenia ya 8 KK.

Katika milenia ya 5 KK watu walizidi kuhama Sahara ikigeuka jangwa wakasogea katika eneo la Sudan ya sasa (bonde la mto Nile).

Mchanganyiko wa watu hao uliunda ufalme wa Kush kwenye 1700 KK. Makao makuu yalikuwa Kerma.

Katika karne ya 8 KK watu wa ufalme huo waliteka Misri na kuitawala kwa karne moja hadi waliposhindwa na Waashuru.

Baadaye makao makuu yalikuwa Meroe, ambapo ufalme uliendelea hadi karne ya 4 BK ukiwa maarufu kwa uhunzi kwa jina la Ethiopia.

Ufalme kusambaratika[hariri | hariri chanzo]

Ufalme huo uliposambaratika, zilitokea falme mbalimbali katika eneo lake, mmojawapo ukiwa ule wa Nubia.

Huko Ukristo ulienea katika madhehebu tofauti: yale ya Kikopti kutoka Misri na yale ya Kibizanti kutoka Roma ya mashariki.

Baadaye Uislamu pia ulijitokeza katika falme hizo ukazidi kuenea hadi kuanzisha usultani wa Sennar.

Mwaka 1821 mtawala wa Misri chini ya himaya ya Waturuki aliteka Sudan kaskazini.

Katika miaka ya 1870 juhudi za Wazungu za kukomesha biashara ya utumwa zilisababisha kutokea kwa Mahdi.

Dola la Mahdi[hariri | hariri chanzo]

Dola la Mahdi (kwa Kiarabu المهدية, "mahdiyya") lilianzishwa na Muhammad Ahmad Al-Mahdi mwaka 1881 alipojitangaza kuwa mahdi kufuatana na imani ya Kiislamu akaongoza uasi dhidi ya Misri iliyotawala Sudan ikisimamiwa yenyewe na Uingereza.

Muhammad Ahmad Al-Mahdi alifaulu kukusanya wafuasi wengi na kushinda Wamisri. Tarehe 26 Januari 1885 jeshi lake lilitwaa mji mkuu Khartum na kumwua gavana Gordon Pasha.

Al-Mahdi alianzisha mji mkuu mpya ng'ambo ya mto Nile kwa kuunda Omdurman. Wamisri na Waingereza wakatoka nje ya Sudan.

Baada ya ushindi wake Al-Mahdi alikufa na homa ya matumbo.

Ugomvi ulitokea kati ya makamu wake hadi 1891 wakati Abdallahi ibn Muhammad mwenye sifa ya kuwa aliongoza jeshi la mahdi wakati wa mashambulio dhidi ya Khartum alikubaliwa wa viongozi wa mahdiyya akajiita "khalifa".

Khalifa Abdullahi aliimarisha utawala wake wa kuwaua wapinzani bila neema, kati yao wanafunzi na ndugu za mahdi mwenyewe. Akajenga jumba mjini Omdurman linalosimama hadi leo.

Khalifa Abdullahi alijaribu kutumia teknolojia mbalimbali. Akanunua meli za mvuke za mtoni alizoziona Waingereza walizitumia pia akajenga kiwanda cha kutengenezea bunduki. Akaanzisha nyaya za mawasilaino kwa simu. Lakini kwa ujumla vita na utawala wa mahdiyya zilikuwa ziliharubu uchumi iliyoendelea kuzorota.

Khalifa alifaulu kupanua utawala wake juu ya maeneo karibu yote ya Sudan ya leo lakini alishindwa kufikia jimbo la Ikweta ambako Emin Pasha aliendelea kutetea mabaki ya Sudani ya Kimisri.

Jeshi la Mahdiyya

Itikadi ya kupanua utawala wa mahdiyya kwa njia ya jihad ilimsababisha khalifa kushambulia nchi jirani ya Ethiopia iliyotawaliwa na kaisari wa Kikristo. Mwaka 1887 akaongoza jeshi la askari 60,000 hadi Gondar. Waethiopia wakajibu kwa kushambulia Sudan mwaka 1889. Kifo cha Kaisari Yohane IV katika mapigano ya Metemma tarehe 9 Machi 1889 ililazimisha Waethiopia kurudi kwao. Lakini jeshi la mahdiyya lilipoteza wanajeshi wengi pia likadhoofika.

Wakati huohuo jemadari wa khalifa Abd ar-Raħmān an-Nujumī alishambulia Misri lakini alishindwa kwenye mapigano ya Tushkah. Hii ilikuwa mara ya kwanza ya jeshi la mahdiyya kushindwa.

Majaribio ya vita za jihadi dhidi ya Wabelgiji katika jimbo la Ikweta na dhidi ya Waitalia katika Eritrea yalishindikana pia.

Mapigano ya Omdurman 2 Septemba 1898

Mwaka 1895 mkuu wa jeshi la pamoja la Misri na Uingereza, jenerali Horatio Kitchener aliamua kulipiza kisasi kwa vita ya 1885 akaongoza jeshi kubwa dhidi ya Sudan. Kwa kutumia meli za mvuke kwenye mto Nile na kujenga reli akasongea mbele hadi Omdurman.

Tarehe 2 Septemba 1898 jeshi la mahdiyya lilishindwa kabisa katika mapigano ya masaa matano. Safari hiyo Waingereza waliandaliwa vizuri zaidi, pia silaha mpya kama bunduki ya mtombo ziliwapa ushindi. Upande wa khalifa walikufa askari 11,000, upande wa Waingereza na Wamisri watu 400 pekee.

Khalifa mwenyewe alitoroka akajenga jeshi upya na kutawala kusini mwa Sudan, lakini akauawa mwaka 1899 katika mapigano ya Umm Diwaykarat.

Hivyo Waingereza walitawala Sudan pamoja na Misri hadi 1956, na Kitchener akawa gavana mkuu wa kwanza.

Matatizo na vita[hariri | hariri chanzo]

Ramani ya siasa ya Sudan kabla ya Sudan Kusini kujitenga.

Baada ya uhuru wa nchi (1956), makabila ya kusini yalipigania vita ndefu hadi kupata uhuru wao.

Darfur ni eneo yenye majimbo matatu ambaye imeathiriwa na vita vya kisiasa, vita vya Darfur.

Pia kuna wanamgambo upande wa mashariki Umbele wa Mashariki.

Watu na makabila[hariri | hariri chanzo]

Kadiri ya sensa za mwaka 1993, wakazi walihesabiwa kuwa milioni 26. Hakuna sensa nyingine ya hakika iliyofanyika baada ya mwaka huo kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kadirio ni kwamba wakazi ni milioni 37.3 mwaka 2014.

Umma wa miji kama Khartoum (na pia Khartoum, Omdurman, na Khartoum ya kaskazini) waongezeka zaidi: umma wa miji hii yakadiriwa milioni 6-7 na wengine wahamiaji milioni 2 ambao wamekimbia vita vya kusini, magharibi, mashariki na pia wengine kwa sababu ya ukame.

Sudan ina aina mbili za utamaduni — Waafrika walio na Uarabu na Waafrika wasio Waarabu — na maelfu ya makabila na migao ya kabila, lugha tofautitofauti kwa makundi au kabila – migawanyiko hii uleta siasa za utengo na ubaguzi.

Majimbo ya Kaskazini hasa ndio makubwa nchini Sudan, na pia miji mikubwa iko katika majimbo haya. Zaidi ya milioni 22 wanaoishi katika majimbo haya ni Waislamu-Waarabu na wanaongea Kiarabu, lakini wengi pia huongea lugha 70 za kikabila hasa Kinubi, Kibeja, Kifur, Kinuban, Kiingessana, kwa kikundi hiki kuna wale wavutia zaidi kama: Wa-Kababish kutoka kaskazini Kordofan, watu hawa wanaofuga ngamia; Ga’alin (الجعلين), Rubatab (الرباطاب), Manasir (المناصير) and Shaiqiyah (الشايقيّة); makabila ambao kikao chao ni karibu na mito ni kama Baggara wa Kurdufan na Darfur; Wakiham Beja eneo ya bahari ya Shamu na Wanubi wa kaskazini Nile, ambao wengine wamehamishwa karibu na mto Atbara. Eneo la Shokrya kwa Wa-butana, Wa-bataheen wamepakana na Waga’alin na Washorya, upande wa kusini-magharibi eneo ya Butana. Pia kuna Warufaa, Wahalaween na makabila mengine mingi eneo la Gazeera na kwa ufuo wa Bluu Nile na eneo ya Dindir. Hata Wanubi kusini mwa eneo la Kurdufan na Wafur upande wa magharibi.

Makabila[hariri | hariri chanzo]

(zaidi, eneo ambazo zimechapika)

  • Nyingine zaidi

Utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Dini[hariri | hariri chanzo]

Dini kubwa zaidi nchini ni Uislamu (97%).

Wakristo ni waumini hasa wa Kanisa Katoliki, Anglikana (Kanisa la Sudan), Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki (Wakopti, Waethiopia na Waeritrea).

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Vyuo Vikuu vya Sudan:

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Maarifa ya Kawaida

<!—Tafadhali usiweke maadishi au kifungu kuhusu biashara hapa, kwa mfano; vitabu vya Sudan --> <!—Ukiweka maadishi hayo, waweza KUFUNGIWA kuhariri Wikipedia! -->

Serikali

Habari

Picha

(Sura mpay ya sudan)

Utalii

Nyingine


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia
Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sudan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.