Bunge

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Bunge ni chombo cha kutunga sheria na pia ni mmoja wa mihimili mitatu inayounda mfumo wa utawala kulingana na mgawanyo wa madaraka. Mihimili mingine ni mahakama na serikali.

Bunge ni chombo kinachotokana na mfumo wa utawala wa Westminster, ambao umerithiwa na nchi nyingi duniani kutoka Uingereza. Kutokana na mfumo huo kuenea, mara nyingi Bunge la Uingereza huitwa "Mama wa Bunge" duniani.

Bunge la kwanza nchini Uingereza liliundwa wakati wa utawala wa Mfalme Henri III katika karne ya 13. Bunge hilo lina sehemu mbili, Bunge la Makabwela na Bunge la Mabwanyeye.

Katika nchi nyingi zinazofuata mfumo wa Westminster, Waziri Mkuu huwa ndio kiongozi mkuu wa serikali bungeni.

Shughuli za bunge husimamiwa na mbunge aliyechaguliwa kama mwenyekiti, rais au spika wa bunge.

Mabunge ya Afrika[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]