Dominica

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Commonwealth of Dominica
Bendera ya Dominica [[Picha:|110px|Nembo ya Dominica]]
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Après le Bondie, C'est la Ter (Kifaransa)
(Baada ya Mungu ni dunia)
Wimbo wa taifa: Isle of Beauty, Isle of Splendour
Lokeshen ya Dominica
Mji mkuu Roseau
15°18′ N 61°23′ W
Mji mkubwa nchini Roseau
Lugha rasmi Kiingereza
Serikali Demokrasia
Nicholas Liverpool
Roosevelt Skerrit
Uhuru
Tarehe

3 Novemba 1978
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
751 km² (ya 184)
1.6
Idadi ya watu
 - Agosti 2006 kadirio
 - 2001 sensa
 - Msongamano wa watu
 
68,902 (ya 2011)
69,625
105/km² (ya 95)
Fedha East Caribbean Dollar (XCD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-4)
(UTC-4)
Intaneti TLD .dm
Kodi ya simu +1-767

-

1Rank based on 2005 UN estimate.


Ramani ya Dominica.

Dominica ni nchi ya kisiwani katika Bahari ya Karibi. Haitakiwi kuchanganywa na Jamhuri ya Dominika ambayo ni nchi nyingine katika Karibi.

Jina limetokana na lugha ya Kilatini na linamaanisha „Jumapili“ kwa sababu Kristoforo Kolumbus alifika hapa mara ya kwanza siku ya Jumapili tarehe 3 Novemba 1493.

Nchi ni mwanachama wa Jumuiya ya Madola, lakini ni jamhuri.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Dominica ilikuwa kati ya visiwa vya mwisho katika Karibi vilivyotekwa na Wazungu kutokana na utetezi mkali wa wenyeji Waindio. Ni pia mahali pa mwisho ambako bado wako Wakaribi waliopotea penginepo kwenye visiwa vya Karibi.

Tabia ya kisiwa kuwa na milima mingi kwa muda mrefu haikuonekana ni mahali pazuri pa kilimo ya mashamba makubwa. Hivyo mataifa yaliyounda makoloni kwa muda mrefu hayakuvutwa kulipa gharama za kupeleka wanajeshi wengi kisiwani waliohitajika kukandamiza Waindio.

Hispania iliacha majaribio ya kuteka kisiwa katika karne ya 16.

Uingereza ilijaribu kuunda utawala wake juu ya kisiwa mwaka 1627 ikaacha.

Mwaka 1635 Ufaransa ilipeleka bendera yake Dominica lakini ikaacha pia.

Tangu mwaka 1748 Uingereza na Ufaransa walipatana ya kwamba kisiwa kitakuwa eneo lisilotawaliwa na upande moja.

Katika miaka iliyofuata walowezi wachache Wafaransa walianzisha mashamba na mji wa Roseau.

Baada ya vita ya miaka saba Uingereza ulichukua utawala wa kisiwa na kupeleka walowezi pamoja na watumwa kutoka Afrika kisiwani. Waindio walirudishwa polepole katika maeneo ya milimani.

Uhuru ulipatikana tarehe 3 Novemba 1978.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Kisiwa kina urefu wa km 46.4 na upana wa km 25.6, eneo lake ni km² 746.

Mlima mkubwa ni volkeno ya Morne Diablotins yenye kima cha m 1,447 juu ya UB.

Kuna misitu mingi na maeneo ya kuhifadhiwa.

Miji[hariri | hariri chanzo]

Miji mikubwa zaidi kisiwani ni:

  • 1. Roseau: wakazi 16,571
  • 2. Portsmouth: wakazi 3,633
  • 3. Marigot: wakazi 2,669
  • 4. Berekua: wakazi 2,608
  • 5. Mahaut: wakazi 2,369
  • 6. Saint Joseph: wakazi 2,184

Watu[hariri | hariri chanzo]

Kwa sasa wakazi 75% wana asili ya Afrika na 19.2% ni machotara.

Lugha rasmi ni Kiingereza, lakini wengine wanazungumza Krioli zinazotegemea Kifaransa.

Upande wa dini, 80% ni Wakatoliki.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Caribe-geográfico.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Dominica kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.