Jamhuri ya Masedonia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Република Македонија
Republika Makedonija

Jamhuri ya Masedonia
Bendera ya Jamhuri ya Masedonia Nembo ya Jamhuri ya Masedonia
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: {{{national_motto}}}
Wimbo wa taifa: Денес над Македонија
Leo juu ya Masedonia
Lokeshen ya Jamhuri ya Masedonia
Mji mkuu Skopje (tamka: "skopye"
42°0′ N 21°26′ E
Mji mkubwa nchini Skopje
Lugha rasmi Kimasedonia1
Serikali Parliamentary Jamhuri
Gjorge Ivanov
Nikola Gruevski
Independence
Ilitangazwa
8 Septemba 1991
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
25,333 km² (ya 148)
1.9
Idadi ya watu
 - 2011 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
2,058,539 (ya 146)
80.1/km² (ya 122)
Fedha Denar ya Masedonia (MKD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD .mk
Kodi ya simu +389

-

1Kimasedonia ndiyo lugha rasmi. Kila lugha inayotumiwa na 20% ya wakazi hutumiwa kama lugha rasmi ya nyongeza kimahalI kama vile Kialbania, Kituruki, Kiromany na Kiserbia.


Ramani ya Jamhuri ya Masedonia

Jamhuri ya Masedonia (kwa Kimasedonia Република Македонија / Republika Makedonija) ni nchi kwenye rasi ya Balkani katika Ulaya ya kusini mashariki. Imepakana na Serbia, Albania, Ugiriki na Bulgaria.

Mji mkuu ni Skopje, wenye wakazi 600,000. Miji midogo zaidi ni pamoja na Bitola, Prilep, Tetovo, Kumanovo, Ohrid, Veles, Štip, Gostivar na Strumica.

Masedonia ni nchi mwanachama ya Umoja wa Mataifa na inasubiri kupokewa katika Umoja wa Ulaya.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Masedonia ya Kale[hariri | hariri chanzo]

Katika karne za kabla ya Kristo Masedonia ilikuwa eneo la kaskazini la Ugiriki. Wakazi wake wanaaminiwa walisema lahaja za Kigiriki, lakini mara nyingi hawakutambuliwa na Wagiriki wenyewe kama wenzao, jinsi tunavyojua kutoka waandishi wa Ugiriki ya Kale.

Mnamo 500 KK kulikuwako Jina rasmi la kimataifa ni "'''Masedonia iliyokuwa jamhuri ya Yugoslavia'''" (tazama chini). ufalme ulioitwa Masedonia na wafalme waliruhusiwa kwenye michezo ya Olimpiki ya madola ya Wagiriki.

Pamoja na sehemu nyingi za Ugiriki ufalme huo ulipaswa kukubali ubwana wa Milki ya Uajemi, lakini mfalme Filipo II wa Masedonia alifaulu, kuanzia mnamo mwaka 360 KK, kurudisha uhuru wa ufalme akaendelea kuifanya Masedonia kuwa dola kiongozi kati ya madola madogo ya Ugiriki.

Mwanawe Aleksander aliimarisha utawala wake juu ya Wagiriki wengine na kushambulia Milki ya Uajemi na hatimaye kuivamia na kuishinda kwa jeshi la Wagiriki kutoka sehemu zote.

Mnamo mwaka 325 KK mfalme wa Masedonia alitawala nchi zote kuanzia Ugiriki hadi Misri, Syria, Uajemi, mipaka ya Uhindi na Asia ya Kati.

Baada ya kifo cha Aleksander mnamo 323 KK milki yake iligawiwa, na Masedonia ilikuwa tena ufalme wa pekee. Ikaendelea kwa kujitegema hadi uenezi wa Dola la Roma ikawa jimbo la Kiroma tangu mwaka 147 KK.

Baadaye ufalme wa awali iligawiwa kwa majimbo mbalimbali. Wakazi walibadilika polepole kutokana na uhamiaji ndani ya Dola la Roma.

Kufika kwa Waslavoni[hariri | hariri chanzo]

Tangu karne ya 6 BK makabila ya Waslavoni yalifika katika sehemu zilizowahi kuitwa Masedonia zamani. Sehemu kubwa ya eneo ilikuwa chini ya milki ya Wabulgaria, tangu 1018 sehemu ya jimbo la Bulgaria katika Milki ya Bizanti.

Mnamo 1392 Waturuki Waosmani walianza kuvamia Masedonia iliyoendelea kukaa chini ya Milki ya Osmani hadi 1912.

Masedonia ya kisasa[hariri | hariri chanzo]

Sehemu kubwa ya Masedonia ya Kale leo hii iko ndani ya Ugiriki na pia Bulgaria. Jamhuri ya leo ina tabia ya pekee kwa sababu ilikuwa sehemu ya Yugoslavia hadi 1991.

Masedonia ni eneo linalokaliwa hasa na Waslavoni wanaozungumzwa lugha iliyo karibu na Kibulgaria na pia Kiserbia. Eneo hili lilitawaliwa kwa muda mrefu na Dola la Uturuki. Si rahisi kujua watu wa sehemu hizi walianza lini kujisikia kama watu tofauti na wa pekee na majirani yao hasa Wabulgaria. Inaonekana hii ilitokea hasa wakati wa karne ya 20.

Masedonia ya leo ilikuwa jimbo la kujitawala la Yugoslavia. Baada ya mwisho wa shirikisho la Yugoslavia, Masedonia nayo ilitafuta uhuru wake.

Mwanzoni palikuwa na matatizo ya kutumia jina hilo kwa sababu ya upinzani wa Bulgaria na Ugiriki zinazodai kuwa "Masedonia" ni sehemu ya urithi wao wa kitaifa. Kwa muda nchi ilijulikana rasmi kama "Masedonia iliyokuwa jamhuri ya Yugoslavia" lakini yenyewe iliamua kujiita "Jamhuri ya Masedonia" tu.

Wakazi na utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Wamasedonia Waslavoni ni takriban theluthi mbili za wakazi wote. Robo moja ni Waalbania. Wengine ni mchanganyiko wa vikundi vidogovidogo kama Waturuki, Waromany na Waserbia.

Wamasedonia wenyewe ni hasa Wakristo Waorthodoksi (64.7% za wakazi wote). Waalbania na Waturuki ni hasa Waislamu (33.3%). Lakini zaidi ya theluthi ya watu wote husema ya kwamba hawana dini. Hii inaaminiwa ni urithi wa kipindi cha ukomunisti nchini.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Jamhuri ya Masedonia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.