Anwani ya kijiografia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Anwani ya kijiografia ni namna ya kutaja mahali duniani. Anwani ya kijiografia huelezwa kwa kutaja longitudo na latitudo za mahali fulani.

Dunia hugawiwa katika gredi 360 za longitudo na gredi 180 za latitudo (90° za kaskazini na 90° za kusini).

Latitudo za kaskazini na kusini ya ikweta zinatofautishwa ama kwa kuongeza herufi "N" (=north au kaskazini) na "S" (south au kusini) au kwa alama za "+" (kaskazini) na "-" (kusini).

Gredi za longitudo zinaanza kuhesabiwa kwenye meridiani ya 0° iliyokubaliwa ni mstari kutoka ncha ya kaskazini hadi ncha ya kusini unaopita katika mji wa Greenwich (karibu na London / Uingereza).

Kwa mfano anwani ya Accra (Ghana) ni: 5°30' N (latitudo) na 0°10' W (longitudo).

Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Anwani ya kijiografia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.