Bahari ya Shamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Eneo la Bahari ya Shamu ("Red Sea")

Bahari ya Shamu (Kiingereza Red Sea, Kiarabu البحر الأحمر Baḥr al-Aḥmar, al-Baḥru l-’Aḥmar; Kiebrania ים סוף Yam Suf; Kitigrigna ቀይሕ ባሕሪ QeyH baHri) ni ghuba kubwa ya Bahari ya Hindi. Jina la kihistoria katika lugha ya Kigiriki ilikuwa Bahari ya Eritrea (ερυθρά θάλασσα, erythrá thálassa).

Kaskazini ni rasi ya Sinai pamoja ghuba ndogo za Aqaba na Suez halafu imeunganika na Mediteranea kwa njia ya Mfereji wa Suez. Kusini Bahari ya Shamu imeunganika na Bahari Hindi kwa njia ya mlango wa bahari wa Bab el Mandeb.

Ghuba yote ina urefu wa takriban 2000 km; upana wake ni kati ya 300 km na 20 km tu kwenye Bab el Mandeb. Eneo lake ni 450,000 km². Vilindi vyake vinaelekea hadi 2500 m chini ya uwiano wa bahari. Vilindi hivi ni sehemu ya Bonde la Ufa. Halijoto ya maji ni kati ya 21-25 °C.

Nchi za kando[hariri | hariri chanzo]

Nchi zinazopakana na Bahari ya Shamu ni: