Kirgizia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Кыргыз Республикасы
Kyrghyz Riespublikasy
Кыргызская Республика
Kyrgyzskaya Respublika

Kyrgyz Republic Кыргызстан
Kirgizia
Bendera ya Kirgizia Nembo ya Kirgizia
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: --
Wimbo wa taifa: Wimbo la Taifa la Kirgizia
Lokeshen ya Kirgizia
Mji mkuu Bishkek
42°52′ N 74°36′ E
Mji mkubwa nchini Bishkek
Lugha rasmi Kikirgizi, Kirusi
Serikali Jamhuri
Kurmanbek Bakiyev
Daniar Usenov
Uhuru
ilitangazwa
Ilikamilishwa


31 Agosti 1991
25 Desemba 1991
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
199,900 km² (ya 86)
3.6
Idadi ya watu
 - Julai 2005 kadirio
 - 1999 sensa
 - Msongamano wa watu
 
5,264,000 (ya 111)
4,896,100
26/km² (ya 176)
Fedha Som ya Kirgizia (KGS)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
KGT (UTC+6)
(UTC)
Intaneti TLD .kg
Kodi ya simu +996

-



Kirgizia (Kikirgizi: Кыргызстан (Kyrghyzstan); Kirusi: Киргизия (Kirgizia), pia Kirgiztan, Kirigizistaniau Kigistani) ni nchi ya Asia ya Kati. Imepakana na Kazakhstan, Uzbekistan, Tajikistan na China. Neno "Kyrgyztan" lamaanisha "nchi ya makablia 40" kwa lugha ya Kikirgizi.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Idadi ya wakazi ilihesabiwa 2005 kuwa watu 5,264,000. Takriban 70 % kati yao ni Wakirgizi wenyewe, halafu kuna Warusi (9 %), Wauzbeki (14.5%) hasa katika kusini. Takriban tatu robo ni Waislamu.

Ramani ya Kirgizia

Historia[hariri | hariri chanzo]

Hadi mwaka 1991 Kirgizia ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyet. Ilijulikana kwa jina la "Jamhuri ya Kisovyeti ya Kikirgizi" hadi 1991. Ilipata uhuru wake katika mwendo wa kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti.

Kabla ya uhuru yalitokea mabadiliko katika uongozi wa chama cha kikomunisti. Viongozi wapya waliotafuta njia bila udikteta kali walishika uongozi na rais Askar Akayev alirudishwa madarakani katika uchaguzi wa kwanza na wa pili.

Lakini uchaguzi wa mwaka 2005 ulionekana haukuwa huru na hasira ya wananchi ikalipuka katika mapinduzi. Uchaguzi mpya ukamteua mpinzani wa awali Kurmanbek Bakiyev aliye rais kwa sasa.

Vijisehemu[hariri | hariri chanzo]

Ramani ya mikoa ya Kirgizia

Hii ni orodha ya mikoa ya Kirgizia na miji mkuu:

  1. Bishkek (mji)
  2. Mkoa wa Batken (Batken)
  3. Mkoa wa Chuy (Bishkek)
  4. Mkoa wa Jalal-Abad (Jalal-Abad)
  5. Mkoa wa Naryn (Naryn)
  6. Mkoa wa Osh (Osh)
  7. Mkoa wa Talas (Talas)
  8. Mkoa wa Issyk Kul (Karakol)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China.


BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kirgizia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.