Korea Kusini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
대한민국 Daehan Minguk
Jamhuri ya Korea
Bendera ya Korea ya Kusini Nembo ya Korea ya Kusini
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: 널리 인간을 이롭게 하라 "Lete faida kwa watu wote"
Wimbo wa taifa: Aegukga
(Wimbo la Taifa)
Lokeshen ya Korea ya Kusini
Mji mkuu Seoul
37°35′ N 127°0′ E
Mji mkubwa nchini Seoul
Lugha rasmi Kikorea
Serikali Jamhuri
Park Geun-hye
Jung Hong-won
Kuundwa kwa
Ufalme wa Gojoseon
Tangazo la uhuru bado chini ya Japani
Ukombozi kutoka utawala wa Japani
Jamhuri ya kwanza
ilitambuliwa na Umoja wa Mataifa

3 Oktoba 2333 KKa
1 Machi 1919
15 Agosti 1945
15 Agosti1948
12 Desemba 1948
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
99,646 km² (ya 108)
0.3
Idadi ya watu
 - Julay 2006 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
48,846,823 (ya 25)
480/km² (ya 19)
Fedha Won ya Korea Kusini (KRW)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
Wakati sanifu wa Korea (UTC+9)
-- (UTC+9)
Intaneti TLD .kr
Kodi ya simu +82

-


Ramani ya Korea ya Kusini

Korea ya Kusini (rasmi: Jamhuri ya Korea) ni nchi ya Asia ya Mashariki iliyopo katika kusini ya rasi ya Korea. Upande wa kaskazini imepakana na Korea ya Kaskazini. Korea zote mbili zilikuwa nchi moja hadi 1945 chini ya utawala wa kikoloni wa Japani. Ng'ambo ya bahari iko Uchina upande wa magharibi na Japani upande wa kusini-mashariki.

Mji mkuu pia mji mkubwa ni Seoul ambako karibu nusu ya wakazi wote huishi ama mjini au katika mazingira yake. Seoul ni kati ya miji muhimu ya biashara na uchumi wa kimataifa.

Korea ni kati ya tamaduni za kale duniani. Tangu maungano ya kitaifa ya Korea yote manmo mwaka 668 KK ilikuwa nchi moja hadi 1910 ilifanywa koloni ya Japani. Uhuru baada ya 1945 ilifuatwa na mgawanyiko wa nchi na kuundwa kwa Korea Kusini. Awali ilikuwa nchi maskini yene uchumi w kilimo lakini iliendelea kuwa nchi ya viwanda iliyofaulu kusogea mbele na kujenga demokrasia imara.

Siku hizi imekuwa moja ya nchi tajiri ya Asia inanafasi ya 13 duniani kati ya mataifa matajiri. Iko kati ya nchi kumi duniani zinazouza bidhaa nyingi nje. Hali ya maisha ni ya juu na viwanda vyake vinatengeneza bidhaa za kisasa kabisa kama motokaa, meli, mashine, vifaa vya kompyuta na mengine.

Dini[hariri | hariri chanzo]

Kiasili watu wa Korea walifuata dini ya jadi iliyoheshimu mapepo mbalimbali na kutoa sadaka kama njia za kuyapatanisha.

Tangu karne ya 4 Ubuddha uliingia kutoka China ukawa dini rasmi. Ukonfusio ulifuata tangu karne ya 13. Ukristo ulingia pia kutoka China ukaanza kukua tangu karne ya 19.

Siku hizi takriban nusu ya Wakorea wa kusini wasema hawana dini. Sehemu kubwa wanakadiriwa kuwa wafuasi wa Konfusio lakini hawajiiti "dini".

Ukristo ni kundi kubwa la kidini ni 29% za Wakorea wa Kusini. Wabuddha ni kama 23 %kunapia wafuasi wachache wa dini mmbalimbali.

Miji[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China.


WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: