Jibini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Soko la jibini mjini Gouda (Uholanzi)
Kiwanda cha jibini ya Parmegiano (Italia)
Aina za jibini huko Basel (Uswisi)

Jibini ni chakula kutokana na maziwa.

Maziwa ya ng'ombe, kondoo au mbuzi hugandishwa. Hupikwa katika sufuria na dawa asilia kutoka tumbo la ng'ombe humwagwa humo pamoja na chumvi. Maziwa yanaganda mara moja na kumwagwa katika kitambaa ili majimaji yatoke na sehemu imara pekee ibaki.

Jibini bichi inaweza kukandamizwa na kuwa imara zaidi. Baadaye ilhali ni bado laini huwekwa katika bakuli na kupokea umbo lake wakati inaendelea kukauka.

Baadaye inakaa na kuiva. Aina mbalimbali za jibini huiva kwa muda tofautitofauti.

Katika nchi za joto ni vigumu zaidi kutengeneza jibini bila mashine na friji lakini katika nchi nyingi jibini ni sehemu ya utamaduni. Jibini ni chakula bora chenye protini na mafuta sawa na maziwa. Kiuchumi ni muhimu kama njia ya kutunza maziwa kwa miezi mingi.

Nchi kama Uswisi, Uholanzi na Ufaransa ni maarufu kwa aina nyingi za jibini na kila moja ina ladha na rangi tofauti.