Mongolia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Монгул Улс
Mongol Uls

Jamhuri ya Mongolia
Bendera ya Mongolia Nembo ya Mongolia
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: "Dayar Mongol"
Wimbo wa taifa: Bügd Nairamdakh Mongol
Lokeshen ya Mongolia
Mji mkuu Ulaanbaatar
47°55′ N 106°53′ E
Mji mkubwa nchini Ulaanbaatar
Lugha rasmi KiMongolia
Serikali Demokrasia ya kibunge
Tsakhiagiin Elbegdorj
Sükhbaataryn Batbold
Uhuru
Kutangazwa
Kutoka Uchina
11 Julai 1921
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
1,564,116 km² (19th)
0.6
Idadi ya watu
 - Julai 2006 kadirio
 - 2000 sensa
 - Msongamano wa watu
 
2,832,224 (139th)
2,650,952
1.8/km² (227th)
Fedha Tugrug (MNT)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+7)
(UTC+8)
Intaneti TLD .mn
Kodi ya simu +976

-



Mongolia (Kimongolia: Монгол Улс  mongol uls) ni nchi katika bara la Asia. Imepakana na nchi za Urusi na Uchina. Ni nchi kubwa ya 19 duniani lakini kuna wakazi wachache tu jumla milioni 2.6 hivyo songamano la watu ni kidogo sana. Sehemu za kusini ya Mongolia ya kihistoria ziko ndani ya Jamhuri ya Watu wa China. Hadi 1992 nchi iliitwa Jamhuri ya Watu wa Mongolia.

Miaka 800 iliyopita nchi hii ilikuwa chanzo cha moja kati ya milki kubwa kabisa katika historia wakati ambako Chingis Khan alipounda Milki ya Wamongolia iliyoenea kuanzia China hadi Mashariki ya Kati na Ulaya.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Ramani ya Mongolia

Mongolia ni nchi ya mbuga yabisi, majangwa na milima inayofikia kimo cha 4,374 m juu ya UB (Nayramadlin Orgil). Kaskazini ya nchi ina ardhi yenye hali ya sakitu ya kudumu yaani yenye halijoto chini ya 0 C° ndani yake isiyopoa hata wakati wa majira ya joto. Kusini kuna jangwa kubwa la Gobi.

Asilimia 10 pekee za nchi ina misitu hasa mlimani na ardhi inayolimika ni 1 % tu.

Hali ya hewa[hariri | hariri chanzo]

Hali ya hewa ni ya kibara ina tofauti kubwa. Majira hubadilishana kuwa na joto pia baridi kali. Wastani ya siku ni kati ya −25 °C na +20 °C. Hali halisi wakati wa joto mchana kuna joto kali lakini usiku huwa baridi.

Usimbishaji una tofauti kubwa kati ya kaskazini na kusini ya nchi. Kusini ni yabisi zaidi hadi kushuka kwa 100 mm za mvua pekee kwa mwaka katika jangla la Gobi.

Miji[hariri | hariri chanzo]

Miji mikubwa ni mji mkuu Ulaanbaatar (Улаанбаатар) (takriban wakazi milioni moja - zaidi ya theluthi ya watu wote wa taifa), halafu Erdenet (wakazi 79,649), Darchan (72,386) na Choibalsan (44,367).

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Uchumi wa Mongolia hutegemea hasa migodi na ufugaji. Kihistoria Wamongolia walikuwa wafugaji waliohamahama na wanayama wao na kuishi katika hema. Tangu mapinduzi ya 1921 sekta ya migodi na viwanda ilijengwa.

Sekta ya kisasa ya kibiashara iko hasa kwenye mji mkuu.

Hadi leo karibu nusu ya wakazi huishi nje ya miji porini wakifuatana na wanyama wao ambao ni hasa kondoo, mbuzi, ng'ombe, farasi na ngamia. Kilimo kipo mahali pachache kufuatana na tabia yabisi ya nchi. Wakati wa baridi sehemu kubwa ya wafugaji hukaa vijijini walipojenga nyumba.

Migodi ni hasa makaa mawe, shaba, bai na dhahabu.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China.


BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mongolia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.