Eire

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Éire
Eire (Ireland)
Bendera ya Eire Nembo ya Eire
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: {{{national_motto}}}
Wimbo wa taifa: Amhrán na bhFiann
"Wimbo wa Askari"
Lokeshen ya Eire
Mji mkuu Dublin
53°26′ N 6°15′ W
Mji mkubwa nchini Dublin
Lugha rasmi Kieire, Kiingereza
Serikali Jamhuri
Michael D. Higgins
Enda Kenny
Uhuru
Ilitangazwa
Ilitambuliwa
Katiba

24 Aprili 1916
6 Desemba 1922
29 Desemba 1937
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
70,273 km² (ya 120)
2.00
Idadi ya watu
 - 2014 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
4,609,600 (ya 121)
65.3/km² (ya 142)
Fedha Euro ()1 (EUR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
WET (UTC+0)
IST (WEST) (UTC+1)
Intaneti TLD .ie2
Kodi ya simu +353

-

1 kabla ya 1999: Irish pound.
2 kuna pia anwani za .eu (Umoja wa Ulaya)Eire (pia: Ireland, Ayalandi; kwa Kiingereza mara nyingi Republic of Ireland) ni nchi ya kisiwani katika funguvisiwa ya Britania ya Ulaya.

Mji mkuu ni Dublin.

Wakazi walio wengi hutumia lugha ya Kiingereza lakini lugha ya Kieire ni lugha ya kwanza ya taifa. Kinazungumzwa katika maeneo kadhaa ya vijijini na hufundishwa shuleni.

Upande wa dini, 74.2% ni Wakatoliki na 4.6% ni Wakristo wa madhehebu mengine. Ushiriki wa ibada ni wa juu sana.

Eire ilitawaliwa na Uingereza hadi mwaka 1922. Sehemu ya kaskazini ya kisiwa imebaki kama sehemu ya Ufalme wa Muungano (Uingereza).

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Kijiografia Eire ni kisiwa kilichogawiwa kati ya Jamhuri ya Eire inayokalia sehemu kubwa ya kisiwa na Northern Ireland ambayo ni jimbo la Ufalme wa Maungano.

Kisiwa chote kina eneo la 84,421 km² na 83% zake ni Jamhuri ya Eire. Upande wa magharibi kuna Bahari ya Atlantiki, upande wa mashariki Bahari ya Eire inayokitenga na kisiwa cha Britannia.

Kitovu cha kisiwa kuna tambarare inayozungukwa nje upande wa pwani na vilima.

Mlima mkubwa ni Carrauntoohil wenye kimo cha mita 1,038.

Mto mkubwa ni Shannon ambao unaelekea kutoka kaskazini kwenda kusini. Kwenye tambarare ya katikati kuna maziwa kadhaa.

Hali ya hewa inaathiriwa na Atlantiki: ni ya wastani, hakuna baridi kali wala joto kali.

Bahari inaleta mvua nyingi na hivyo Eire huitwa "Kisiwa cha Kijani".

Miji mikubwa ni Dublin (wakazi milioni 1), Cork (watu 190,000), Limerick (90,000), Galway (72,000) na Waterford (49,000).

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Denmark | Estonia | Hispania | Hungaria | Ireland | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituania | Luxemburg | Malta | Poland | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Ufalme wa Muungano | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Ireland smaller.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Ireland bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Eire kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.