San Marino

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Serenissima Repubblica di San Marino
Jamhuri ya kuheshimiwa ya San Marino
Bendera ya San Marino Nembo ya San Marino
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Kilatini: Libertas
("Uhuru")
Wimbo wa taifa: Inno Nazionale della Repubblica (sauti pekee bila maneno)
Lokeshen ya San Marino
Mji mkuu San Marino
43°56′ N 12°27′ E
Mji mkubwa nchini Serravalle
Lugha rasmi Kiitalia
Serikali
Watawala wakuu(Capitani Reggenti)
Jamhuri
Valeria Ciavatta
na Luca Beccari
Uhuru
imeundwa
3 Septemba, 301
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
61 km² (190th)
kidogo sana
Idadi ya watu
 - 31 Julai 2012 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
32,576 (ya 190)
520/km² (ya 13)
Fedha Euro (€) (EUR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD .sm
Kodi ya simu +378 (0549 kutoka Italia)

-



San Marino (kwa Kiitalia maana yake ni "Mtakatifu Marino") ni kati ya nchi ndogo kabisa duniani. Eneo lake lote limo ndani ya mipaka ya Italia, kati ya wilaya za Rimini na Pesaro-Urbino, karibu na mwambao wa bahari ya Adria.

San Marino inatajwa kuwa jamhuri yenye umri mkubwa duniani. Ilianzishwa na Wakristo waliokimbia dhuluma ya Kaisari wa Roma Diokletiano wakitafuta kimbilio mlimani.

Kati yao, shemasi Marino na padri Leo ndio mmarufu zaidi.

San Marino ina wakazi 32,576 hivi katika vijiji 9. Karibu wote (97.2%) ni waumini wa Kanisa Katoliki (jimbo la San Marino-Montefeltro) na wanaongea Kiitalia kwa lahaja ya Kiromagna.

Eneo lote la km² 61 ni la milima.

Siasa[hariri | hariri chanzo]

San Marino imetunza utaratibu wa serikali inayofanana na muundo wa jamhuri ya Roma ya kale. Serikali inaongozwa na watawala wawili ("Capitani Reggenti") wanaochaguliwa kwa muda wa miezi sita tu kama zamani konsuli wa Kiroma.

Bunge linaitwa Halmashauri Kuu ("Consiglio Grande e Generale") likichaguliwa kila baada ya miaka mitano. Halmashauri inateua pia kamati ya watu 12 ("Consiglio dei XII") inayotekeleza kazi ya mahakama.

Wananchi wote hukutana mara mbili kwa mwaka kama mkutano mkubwa wa "Arengo" wakiamua juu ya matamko na mapendekezo kwa serikali.

Mtazamo kutoka San Marino hadi bahari ya Adria
Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu San Marino kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.