Funguvisiwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Funguvisiwa ya Hawaii katika Pasifiki

Funguvisiwa ni kundi la visiwa vinavyokaa sehemu pamoja baharini. Mara nyingi kundi hili lina asili ya pamoja, kama vile kuwa mabaki ya kisiwa kikubwa zaidi kilichogawiwa kutokana mmomonyoko wa ardhi yake au kuwa na asili ya kivolkeno.

Atolli inaweza kuonekana pia kama kundi la visiwa lakini huhesabiwa zaidi kama kisiwa kimoja hata kama sehemu kadhaa ziko chini ya maji. Bahari za Pasifiki na Bahari Hindi kuna funguvisiwa za atolli.

Funguvisiwa kubwa kabisa duniani ni Indonesia pamoja na Ufilipino inayoitwa pia Fungusiwa ya Malay.

Bahari ya Pasifiki ina funguvisiwa nyingi, pia sehemu ya Karibi ya Bahari ya Atlantiki karibu na Amerika ya Kati.

Funguvisiwa muhimu za Afrika ni Zanzibar, Shelisheli na Komoro katika Bahari Hindi, halafu katika Atlantiki Visiwa vya Kanari na Visiwa vya Madeira.

Funguvisiwa ndogo karibu na pwani la Afrika ya Mashariki ziko Lamu, Kilwa na Kirimba.