Haiti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Krioli: Repiblik d Ayiti
Kifaransa: République d'Haïti''

Jamhuri ya Haiti
Bendera ya HaitiF Nembo ya HaitiF
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: L'Union Fait La Force
("Umoja ni nguvu")
Wimbo wa taifa: La Dessalinienne
Lokeshen ya HaitiF
Mji mkuu Port-au-Prince
18°32′ N 72°20′ W
Mji mkubwa nchini Port-au-Prince
Lugha rasmi Kifaransa na Kikreoli cha Haiti
Serikali Jamhuri
Michel Martelly
Evans Paul
Uhuru
kutoka Ufaransa
1 Januari 1804
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
27,750 km² (ya 147)
0.7
Idadi ya watu
 - Julai 2014 kadirio
 - 1982 sensa
 - Msongamano wa watu
 
9,996,7311 (ya 84)
5,053,792
350.27/km² (ya 32)
Fedha Gourde (HTG)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-5)
(UTC-4)
Intaneti TLD .ht
Kodi ya simu +509

-


Ramani ya Haiti

Haiti ni nchi kwenye kisiwa cha Karibi cha Hispaniola. Eneo la Haiti ni takriban theluthi moja ya Hispaniola yote. Sehemu kubwa ya kisiwa ni nchi jirani ya Jamhuri ya Dominika.

Mji mkuu ni Port-au-Prince.

Haiti ni nchi ya kwanza duniani ambako watumwa wenye asili ya Afrika walifaulu kupindua utumwa na kujipatia uhuru kutoka Ufaransa mwaka 1804.

Jina la "Haiti" lina asili katika lugha ya Kitaino ya wakazi asilia; linamaanisha "nchi ya milima", na kweli kisiwa kina milima mingi.

Haiti ni kati ya nchi maskini kabisa duniani na nchi maskini zaidi ya Amerika yote.

Nchi ina wilaya kumi.

Wakazi ni milioni 10, lakini wananchi wengine wengi wamehama kutokana na ufukara. Karibu 900,000 wako Marekani, 800,000 wako Dominikana na 300,000 Kuba, halafu Kanada, Ufaransa, Bahamas.

Kuna lugha rasmi mbili: moja ni Kifaransa na nyingine ni Kikreoli ya Haiti ("Kweyol") inayotokana nacho.

Wakazi wengi ni wafuasi wa Yesu Kristo katika Kanisa Katoliki (80%) lakini wengi hufuata vilevile dini ya vudu inayotokana na dini za jadi kutoka Afrika ya Magharibi. Waprotestanti ni 16%.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mianzo na ukoloni wa Hispania[hariri | hariri chanzo]

Wakazi asilia walikuwa Waindio Waarawak. Baada ya kufika kwa Kristoforo Kolumbus na utawala wa Hispania idadi yao ilipungua haraka kutokana na magonjwa ya Ulaya ambayo hawakuzoea na kukosa kinga dhidi yao na pia kutokana kutendewa vibaya kwa unyama na mabwana wapya. Mnamo mwaka 1600 Waindio wachache tu walibaki kutoka malakhi wakati wa Kolumbus wakapotea kabisa kwa njia ya kuoa au kuolewa na wazungu na weusi. Wahispania walianzisha mashamba kwa kazi ya watumwa kutoka Afrika.

Ukoloni wa Ufaransa[hariri | hariri chanzo]

Katika karne ya 17 Wafaransa walifika kisiwani wakanunua theluthi moja ya kisiwa wakaiita "Saint-Domingue" kilichokuwa baadaye Haiti. Wafaransa walileta watumwa wengi kutoka Afrika na kujenga uchumi wa mashamba makubwa hasa ya miwa. Koloni ya Saint-Domingue ilikuwa koloni tajiri ya Ufaransa katika Amerika.

Mapinduzi ya Ufaransa[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa mapinduzi ya Ufaransa 1789 koloni ilikuwa na wakazi wa aina nne:

  • Wazungu hasa Wafaransa waliokuwa mabwana lakini waliokuwa na tofauti kubwa kati yao wengine tajiri sana wengine maskini -jumla takriban watu 32,000
  • chotara na weusi huru ambao walikuwa raia wa daraja ya pili; wengine walikuwa matajiri na mabwana wa mashamba na pia wa watumwa - jumla watu 28,000
  • watumwa wa asili ya Kiafrika - jumla watu 500,000
  • Wamaroni walikuwa watumwa wakimbizi walioishi mlimani katika pori - idadi yao haijulikana hawakuwa wengi.

Mapinduzi ya Ufaransa na kutangaziwa kwa haki za kibinadamu vilisababisha matumaini ya chotara wenye mali ya kukubaliwa kama raia kamili wenye haki ya kupiga kura. Wenyewe hawakutegemea kumaliza utumwa uliokuwa msingi wa uchumi. Lakini matumaini yao yalishindikana wakakataliwa na watawala kisiwani.

Toussaint L'Ouverture kiongozi wa uhuru wa Haiti

Mapinduzi ya Haiti[hariri | hariri chanzo]

Sehemu ya matajiri kati ya Wazungu walitaka kujitenga na Ufaransa kwa msaada wa Uingereza na Hispania wakichukia mapinduzi katika Ufaransa. Watumwa na weusi huru wenye elimu walifuata habari hizi wakaogopa ya kwamba utawala wa mabwana hawa bila sheria za Ufaransa uatkuwa vibaya zaidi kuliko hali jinsi ilivyokuwa wakaanza mapinduzi.

Kiongozi wao alikuwa Toussaint L'Ouverture aliyefaulu kushika serikali ya koloni tangu 1798. Awali alipigania jeshi la Ufaransa; baada ya bunge la Paris kutangaza mwisho wa utumwa alishirikianna na Ufaransa dhidi ya jeshi la mabwana wenye shamba waliotaka kuendeleza utumwa katika nchi ya kujitegemea.

Toussaint L'Ouverture alishinda pia Waingereza waliotaka kuwasaidia wapinzani Wafaransa wa Paris na 1801 akateka kaskazini ya kisiwa iliyokuwa eneo la Kihispania na kutawala Hispaniola yote akitangaza kote mwisho wa utumwa.

Lakini mmnamo mwaka 1802 siasa ya Paris ilibadilika na mtawala Napoleon Bonaparte aliamua kurudisha Hispaniola kwa hali ya awali akatuma jeshi kubwa la askari 40,000. L'Ouverture alikamatwa alipokubali kushauriana na jenerali Mfaransa akapelekwa kama mfungwa Ulaya. Lakini makamu wake Jean-Jacques Dessalines aliposikia khusu mipango ya Ufaransa ya kurudisha utumwa alianza vita upya. Katika vita vikali Wafaransa walishindwa na Dessalines alitangaza uhuru wa koloni tarehe 1 Januari 1804 kwa jina la "Haiti" kama "Jamhuri ya watu weusi".

Vijisehemu vya Haiti[hariri | hariri chanzo]

Wilaya za Haiti
The MINUSTAH in a mission during the 2006 Elections (Photo: Patrick-André Perron
  1. Artibonite (Gonaïves)
  2. Centre (Hinche)
  3. Grand'Anse (Jérémie)
  4. Nippes (Miragoâne)
  5. Nord (Cap-Haïtien)
  6. Nord-Est (Fort-Liberté)
  7. Nord-Ouest (Port-de-Paix)
  8. Ouest (Port-au-Prince)
  9. Sud-Est (Jacmel)
  10. Sud (Les Cayes)





Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Caribe-geográfico.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Haiti kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.