Botswana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Lefatshe la Botswana
Jamhuri ya Botswana
Bendera ya Botswana Nembo ya Botswana
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Pula (Mvua)
Wimbo wa taifa: Fatshe leno la rona
(Nchi hii nzuri ibarikiwe)
Lokeshen ya Botswana
Mji mkuu Gaborone
24°40′ S 25°55′ E
Mji mkubwa nchini Gaborone
Lugha rasmi Kiingereza (rasmi), Kitswana (kitaifa)
Serikali Jamhuri ya kibunge
Ian Khama
Uhuru
Kutoka Uingereza
30 Septemba 1966
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
581,730 km² (48th)
2.6%
Idadi ya watu
 - 2014 kadirio
 - 2011 sensa
 - Msongamano wa watu
 
2,155,784 (145th)
2,038,228
3.4/km² (231th)
Fedha Pula (BWP)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+2)
(UTC)
Intaneti TLD .bw
Kodi ya simu +267

-



Ramani ya Botswana

Botswana ni nchi huru iliyoko Kusini mwa Afrika. Jina rasmi ni Jamhuri ya Botswana.

Mji mkuu wa Botswana ni Gaborone.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]


Botswana haina pwani kwenye bahari yoyote. Imepakana na Zambia, Zimbabwe, Afrika Kusini na Namibia. Mpaka baina ya taifa la Botswana na Zambia ni meta 700 tu na ndio mfupi kuliko mipaka yote ulimwenguni.

Kuna pia feri ya moja kwa moja kati ya Botswana na Zambia kuvuka mto Zambezi.

Jangwa la Kalahari linafunika theluthi mbili za eneo la Botswana.

Moja ya maeneo muhimu nchini Botswana ni delta ya mto Okavango. Delta ya Okavango ni delta kubwa kabisa duniani, maana yake mdomo wa mto si baharini bali kwenye nchi kavu, maji yakiishia jangwani.

Siasa[hariri | hariri chanzo]

Botswana imekuwa na mfumo wa demokrasia kwa miaka mingi, ikiwa na viongozi ambao huchaguliwa kwa kura ya wananchi wote.

Rais wa jamhuri ni Festus Mogae.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Watu wa Botswana hujiita Batswana kutokana na jina la kabila kubwa kabisa nchini (79%). Kuna wakazi takriban milioni 1.6. Kwa sababu nchi ni kubwa msongamano wa watu kwa kilometa za mraba ni 3.4 pekee. Idadi hiyo ndogo imetokana na sehemu kubwa ya nchi hiyo kuwa jangwa.

Lugha inayotumiwa na wakazi walio wengi ni Setswana (Kitswana) pamoja na Kiingereza.

Upande wa dini, wakazi wengi (73%) ni Wakristo, wakiwemo Waprotestanti (66%) na Wakatoliki (7%). Wafuasi wa dini asilia ya Kiafrika ni 6%. Asilimia 20 haina dini yoyote.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Uchumi wa Botswana umekuwa imara kwa miaka mingi na hali ya maisha imeendelea kuwa bora kila mwaka tangu uhuru.

Utajiri wa nchi unatokana hasa na migodi ya almasi, pamoja na machimbo ya shaba na minerali kama vile chumvi.

Watalii wanaongeza pato la taifa hasa kwa sababu ya uzuri wa delta ya Okavango.

Fedha ya Botswana huitwa Pula (yaani mvua). Ina thebe (="ngao") 100.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia
Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Botswana kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.