Wapiga kura wa Ethiopia Jumatatu wanashiriki kwenye uchaguzi wa kitaifa na majimbo, likiwa zoezi ambalo waziri mkuu Abiy Ahmed ameeleza ni ishara ya demokrasia baada ya kuminywa kwa muda mrefu katika taifa hilo la pili kwa wingi wa watu barani Afrika.
Kila mwaka kawaida kuna matukio yanayo chukua sura mpya, Lakini kwa miezi 12 iliyopita kumekuwa na matukio mengi yaliyo badilisha ulimwengu na kuwepo mitizamo tofauti, na hivyo ni vigumu kuamini kuwa hatuko katika utaratibu ambao unaendesha kila kitu kwa wakati mmoja. Lakini hakuna wakati wa kuchoka
Salamu za rambirambi zaendelea kutolewa kote duniani kufuatia kifo cha muasisi wa taifa la Zambia hayati Kenneth Kaunda.
Mkuu wa kijeshi wa Kivu kaskazini amewaamrisha wakazi wa Goma mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuondoka mara moja.
Kila mwaka, familia nchini Marekani zinawaleta majumbani maelfu ya watoto wanaotoka ndani na nje ya nchi kuwalea. Kumleta nyumbani mtoto mgeni inahitaji kumjengea mazoea. Kumleta nyumbani mtoto wa rangi tofauti inaleta changamoto nyingine katika malezi hayo.