Visiwa vya Marshall

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Aolepān Aorōkin M̧ajeļ
Republic of the Marshall Islands
Jamhuri ya Visiwa vya Marshall
Bendera ya Marshall Islands [[Picha:|110px|Nembo ya Marshall Islands]]
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: "Jepilpilin ke ejukaan"
Wimbo wa taifa: Forever Marshall Islands
Lokeshen ya Marshall Islands
Mji mkuu Majuro
7°7′ N 171°4′ E
Mji mkubwa nchini Majuro
Lugha rasmi Marshallese, Kiingereza
Serikali
Kessai Note
Uhuru
kutoka Marekani

21 Oktoba 1986
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
181 km² (ya 213)
‘‘(kidogo sana)’’
Idadi ya watu
 - Julai 2009 kadirio
 - 2003 sensa
 - Msongamano wa watu
 
68,000 (ya 205)
56,429
342.5/km² (ya 28)
Fedha US Dollar (USD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+12)
(UTC)
Intaneti TLD .mh
Kodi ya simu +692

-


RMImap-CIA.jpg

Visiwa vya Marshall ni nchi ya visiwani ya Mikronesia katika Pasifiki ya magharibi. Nchi jirani katika bahari ni Nauru, Kiribati, Shirikisho la Mikronesia na eneo la Marekani la Kisiwa cha Wake.

Atolli ya Majuro ina nafasi ya mji mkuu.

Wakazi ni 68,000, wengi wakiwa wametokana na wenyeji wa kwanza.

Upande wa dini, wengi ni Wakristo, hasa Wakalvini (51.5%), Wapentekoste, Wakatoliki, mbali ya Wamormoni (8.3%).

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Eneo la visiwa vya Marshall ni safu mbili za visiwa au atolli zinazoelea sambamba:

Kwa jumla kuna visiwa na vipande vya atolli 1,150 katika eneo la bahari la km² 1,900,000.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Jina limetokana na nahodha Mwingereza John Marshall aliyetembelea eneo hili mwaka 1788 na kulichora katika ramani. Ingawa visiwa vilikaliwa tayari tangu karne nyingi na watu kutoka Mikronesia lakini jina la Kizungu limebaki kwa ajili ya jumla ya visiwa.

Mwisho wa karne ya 19 Ujerumani ulianzisha ukoloni juu ya visiwa ukaviunganisha kiutawala na Guinea Mpya ya Kijerumani.

Katika vita kuu ya kwanza ya dunia vilitwaliwa na Japani iliyoendelea kutawala visiwa kama eneo lindwa kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa.

Baada ya vita kuu ya pili ya dunia vilikuwa chini ya Marekani.

Mwaka 1979 visiwa vimepata madaraka ya kujitawala na hatimaye kupokea uhuru kufuatana na azimio la Umoja wa Mataifa mwaka 1990.

Majaribio ya kinyuklia[hariri | hariri chanzo]

Kuanzia mwaka 1946 Marekani ilitumia visiwa kwa ajili ya majaribio ya mabomu ya nyuklia.

Hadi mwaka 1958 ilitokea milipuko 6,913 kwenye atolli za Bikini na Eniwetok. Hadi leo kuna wakazi wa visiwa wanavyoteswa na maradhi yaliyosababishwa na mnururisho wa mabomu haya. Bikini haitawezekana kukaliwa na watu kabla ya mwaka 2050, Eniwetok haifai kwa makazi ya binadamu kwa miaka 24,000 inayokuja.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]


Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Visiwa vya Marshall kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Nchi_na maeneo ya Australia na Pasifiki
Australia | Fiji | Guam | Hawaii | Kaledonia Mpya | Kiribati | Kisiwa cha Pasaka | Mikronesia | Nauru | Nyuzilandi | Niue | Pitcairn | Polynesia ya Kifaransa | Palau | Papua Guinea Mpya | Samoa | Samoa ya Marekani | Visiwa vya Cook | Visiwa vya Mariana ya Kaskazini | Visiwa vya Marshall | Visiwa vya Solomon | Tonga | Tuvalu | Vanuatu | Wallis na Futuna